Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais
Tume ya Utumishi wa Umma
Tume ya Utumishi wa Umma imeundwa chini ya Kifungu Na. 9(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298. Tume ilianza kufanya kazi rasmi tarehe 7/1/2004 baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuteua viongozi ( Mwenyekiti, Makamishna na Katibu wa Tume) kusimamia utendaji wake.
Kazi kubwa ya Tume ya Utumishi wa Umma ni kufuatilia na kusimamia uendeshaji wa shughuli za Rasilimali watu katika Taasisi za Umma na kuhakikisha kuwa Utumishi wa Umma unaendeshwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu.
Tume ya Utumishi wa Umma inaendelea kushirikiana na wadau wake wote ili kuhakikisha kuwa Utumishi wa Umma unakuwa mmoja na watumishi wote wana Taratibu za usimamizi, haki na hadhi inayofanana. Kazi hii ni kubwa na inahitaji ushirikiano kutoka kwa wadau wote.
Hivyo, Tume inawaomba wadau wote hasa Waajiri, Mamlaka za Ajira na Nidhamu na watumishi wa umma kutoa ushirikiano kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na maelekezo yanayotolewa kupitia nyaraka mbalimbali za Serikali ili kufikia lengo la kuboresha Utumishi wa Umma nchini.
Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.