Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais
Tume ya Utumishi wa Umma
MAJUKUMU YA TUME YA UTUMISHI WA UMMA
Kifungu cha 10(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 kimeainisha majukumu ya Tume kama ifuatavyo:-
i) Kumshauri Rais kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma katika kutekeleza majukumu yake aliyopewa Kikatiba chini ya Ibara ya 36 kuhusu ujazaji wa nafasi wazi katika Utumishi wa Umma kadri atakavyohitaji;
ii) Kumsaidia Rais kuhusu masuala mbalimbali ya kiutumishi kadri atakavyohitaji;
iii) Kutoa Miongozo na kufuatilia Uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu katika Utumishi wa umma;
iv) Kupokea na kushughulikia rufaa za mashauri yaliyotolewa uamuzi na Mamlaka za Nidhamu;
v) Kuwezesha,kufuatilia na kutathmini utendaji kazi wa Watumishi wa Umma wa ngazi mbalimbali ili uwe na ufanisi na wenye kuzingatia matokeo; na
vi) kuhakikisha kuwa Taratibu za Uendeshaji za Utumishi wa makundi mbalimbali ya kiutumishi zinatayarishwa na kutumika ipasavyo.
Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.