Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Mamlaka ya Tume

 

Kuhakikisha Waajiri na  Mamlaka za Nidhamu katika Utumishi wa Umma zinazingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma, Tume imekabidhiwa  Mamlaka yafuatayo:-

  • Kuwaita viongozi Watendaji na kuhoji utendaji wao kutokana na ushahidi au Malalamiko juu yao
  • Kumchukulia hatua kiongozi Mtendaji yeyote anayeshindwa kumchukulia hatua mtumishi aliye chini yake.
  • Kuitaka Mamlaka yoyote ya Ajira kuwasilisha Tume  taarifa yoyote inayofanyika katika kutekeleza shughuli zake