Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Mawasiliano Serikalini

 

KAZI ZA KITENGO
Kitengo cha Mawasiliano serikalini kina jukumu la kutoa utaalamu na huduma katika masuala ya Mawasiliano na Habari kwa Tume ya Utumishi wa Umma.

 

MAJUKUMU YA KITENGO

  1. Kuzalisha na kusambaza machapisho, nyaraka, makala, vibango ili kuufahamisha umma juu ya sera, mipango, mikakati, utekelezaji na mafanikio ya Taasisi;
  2. Kuratibu taarifa kwa Vyombo vya Habari kuhusu Taasisi;
  3. Kusimamia shughuli za Mahusiano ya Umma na Huduma kwa Wateja;
  4. kushiriki katika mazungumzo, mijadala ya umma na vyombo vya habari juu ya masuala yanayohusu Tume;
  5.  Kuandaa na kutekeleza mkakati ya mawasiliano wa Tume;
  6. Kutangaza shughuli za Tume, programu na sera kupitia vyombo vya habari vya ndani na nje;
  7. Kuratibu na kufanya maandalizi ya warsha, mikutano na makongamano ya Tume;
  8. Kusimamia na kuhuisha maudhui ya tovuti ya Tume pamoja na mitandao mingine ya kijamii ya Tume;
  9. Kuratibu, Kuhudumia na Kusimamia Maktaba ya Tume.