Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Majukumu ya Tume
         Tume ya Utumishi wa Umma ni chombo rekebu kilichoanzishwa kwa mujibu wa Kifungu cha 9(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 [Marejeo ya mwaka 2019]. Majukumu ya Tume yameainishwa katika Kifungu cha 10(1) cha Sheria tajwa hapa juu ambayo yamegawanyika katika maeneo makuu matatu yafuatayo:-

        1. Ushauri

            1.1 Kumshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutekeleza majukumu yake aliyopewa kwa mujibu wa Ibara ya 36 ya Katiba ya Jamhuri ya

                   Muungano wa Tanzania.

  1.2 Kumsaidia Rais katika masuala yote yanayohusu Utumishi kadiri atakavyohitaji.

2. Urekebu (Regulatory Function)

    2.1 Kutoa Miongozo ya masuala ya Ajira na Nidhamu ambayo husaidia kuwa na tafsiri sahihi ya utekelezaji wa Sheria katika Utumishi wa Umma.

    2.2 Kutoa elimu juu ya utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298 [Marejeo ya mwaka 2019].

    2.3 Kufanya Ukaguzi wa masuala ya Rasilimali Watu katika Taasisi za Umma na Idara za zaSerikali.

3. Kuamua rufaa na malalamiko

     Kupokea na kushughulikia rufaa na malalamiko ya Watumishi wa Umma ambao hawakuridhika na uamuzi wa Mamlaka zao za Nidhamu.