Idara ya Ukaguzi wa Uzingatiaji wa Masuala ya Usimamizi wa Rasilimali Watu
Idara ya Ukaguzi wa Uzingatiaji wa Masuala ya Usimamizi wa Rasilimali Watu
Lengo
Kuhakikisha kuwa Sheria ya Utumishi wa Umma inazingatiwa katika Usimamizi wa Utumishi wa Umma.
Idara inatekeleza majukumu yafuatayo-:
1. Kufuatilia uzingatiaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Kanuni zake.
2. Kusanifu, kusimamia na kuhuisha Mfumo wa Ukaguzi wa Uzingatiaji wa Sheria katika Usimamizi wa Utumishi wa Umma.
3. Kuweka Viwango vya Uzingatiaji vya Usimamizi wa Masuala ya Kiutumishi.
4.Kufanya ukaguzi wa Kawaida na Ukaguzi Maalum wa Uzingatiaji wa Sheria katika usimamizi wa masuala ya kiutumishi kwenye Wizara zote, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi za Umma.