Huduma Zitolewazo
Huduma Zitolewazo
Tume inatoa huduma zifuatazo:-
- Kupokea na kuamua rufaa na malalamiko ya Watumishi wa Umma ambao hawakuridhika na uamuzi wa Mamlaka zao za Nidhamu na Ajira
- Kufanya ukaguzi Maalum na wa Kawaida wa uzingatiaji wa Sheria katika usimamizi wa masuala ya kiutumishi
- Kutoa elimu kwa Wadau kuhusu uzingatiaji wa Sheria Kanuni, Taratibu na Miongozo inayosimamia Utumishi wa Umma ikiwemo haki na wajibu wa watumishi wa Umma
- Kuandaa na kusambaza Miongozo ya Uzingatiaji wa masuala ya kiutumishi
- Kuandaa Taarifa za Hali ya Utumishi wa Umma
- Kutoa habari kwa umma kuhusu masuala yanayohusiana na majukumu ya Tume
- Kutoa ushauri wa Kitaalam kuhusu uzingatiaji wa masuala ya kiutumishi kadri Mamlaka mbalimbali zitakavyohitaji
- Kutoa huduma nyingine kama zilivyoainishwa katika Sheria mbalimbali zilizopo