Usimamizi wa Manunuzi
Kitengo kinatekeleza majukumu yafuatayo-:
1. Kutoa ushauri kwa Afisa Masuuli pamoja na Menejimenti ya Tume kuhusu masuala yote ya Ununuzi na Uondoshaji wa Mali.
2. Kuhakikisha Tume inafuata michakato na taratibu za Ununuzi kama Sheria ya Ununuzi wa Umma inavyoelekeza.
3. Kuandaa Mpango wa Ununuzi na Taarifa za utekelezaji.
4. Kununua, Kutunza na Kusambaza vifaa na Huduma kwa ajili ya mahitaji ya Tume.
5. Kuhakikisha Utunzaji na Usambazaji mzuri wa Mali za Tume na kuzisambaza kwa watumiaji kwa wakati.
6. Kutunza na Kuhuisha kumbukumbu za bidhaa, vifaa na mali za Tume.
7. Kuishauri Bodi ya Zabuni ya Tume kama Kanuni na Sheria za Ununuzi wa Umma zinavyoelekeza.
8. Kusaidia Vitengo, Idara na Sehemu tumizi zinapata Thamani ya Fedha ya Ununuzi wa Bidhaa na Huduma, Ubora na kwa wakati; na
9. Kusimamia zoezi la Kuainisha na Uondoshaji wa Mali Chakavu za Tume.