Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais
Tume ya Utumishi wa Umma
Tume ya Utumishi wa Umma imeundwa chini ya Kifungu Na. 9(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298. Tume ilianza kufanya kazi rasmi tarehe 7/1/2004 baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuteua viongozi ( Mwenyekiti, Makamishna na Katibu wa Tume) kusimamia utendaji wake.
Kazi kubwa ya Tume ya Utumishi wa Umma ni kufuatilia na kusimamia uendeshaji wa shughuli za Rasilimali watu katika Taasisi za Umma na kuhakikisha kuwa Utumishi wa Umma unaendeshwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu.
Tume ya Utumishi wa Umma inaendelea kushirikiana na wadau wake wote ili kuhakikisha kuwa U
Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.