Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Uwezeshaji
Uwezeshaji

JUKUMU LA UWEZESHAJI

  • Tume ya Utumishi wa Umma ina jukumu la kufanya uwezeshaji (mafunzo) kuhusu masuala ya kiutumishi kwa Taasisi za Umma kwa mujibu wa Kifungu cha 10(1) (c) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298 (Marejeo ya Mwaka 2019).
  • Lengo la uwezeshaji ni kuboresha kiwango cha uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo katika Utumishi wa Umma ili kupunguza ukiukwaji wa Sheria, malalamiko kutoka kwa watumishi wa Umma na hasara kwa Serikali zinazotokana na gharama za mashauri ya nidhamu au fidia kwa watumishi wanaothibitika kutotendewa haki.
  • Maeneo ya uwezeshaji unaofanywa na Tume ni ushughulikiaji wa mashauri ya nidhamu, rufaa na malalamiko; maadili ya utendaji kazi katika Utumishi wa Umma; pamoja na haki na wajibu wa Waajiri na Waajiriwa.
  • Kila mwaka wa fedha Tume huandaa na kutekeleza mpango kazi wa uwezeshaji (Mafunzo).