TEHAMA
TEHAMA
Lengo
Kutoa utaalam na huduma za matumizi ya TEHAMA kwa Tume.
Kitengo kinatekeleza majukumu yafuatayo-:
- Utekelezaji wa sera ya TEHAMA na Serikali Mtandao.
- Kuishauri Tume kwenye masuala yanayohusu sera zinazohusiana na utekelezaji wa TEHAMA na Serikali Mtandao.
- Kujenga na kuratibu Mfumo Shirikishi wa Usimamizi wa Menejimenti za Taarifa wa Tume.
- Kuhakikisha kuwa vifaa na program zinatunzwa kwa usahihi.
- Kuratibu na kuwezesha ununuzi wa program.
- Kuanzisha na kuratibu matumizi ya mawasiliano ya kielektroniki na kupandisha taarifa kwenye tovuti.
- Kuratibu usanifu wa utekelezaji na usimamizi wa program tumizi na kanzi data ya Tume.
- Kutoa mapendekezo kwa Tume kuhusu maeneo ya kutumia TEHAMA kama nyenzo ya kuboresha utoaji wa huduma.
- Kuandaa mpango mkakati, miongozo na taratibu za uendeshaji wa TEHAMA kwa kushabihiana na sera ya Taifa ya TEHAMA.
- Kushirikiana na UTUMISHI kuandaa viwango vya TEHAMA kwa vifaa na program.
- Kukusanya mahitaji ya mafunzo kuhusu TEHAMA na kuandaa mpango wa mafunzo.
- Kusimamia na kudhibiti vihatarishi vya miundombinu ya TEHAMA na Mifumo ya Menejimenti ya Taarifa.