Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Huduma za Sheria

Kitengo kinatekeleza majukumu yafuatayo:-

  1. Kutoa usaidizi na ushauri wa kitaalamu kwa Idara na vitengo kwenye tafsiri za sharia kwenye maeneo ya masharti ya mikataba, makubaliano ya utendaji kazi, mikataba ya ununuzi, dhamana, dhima, hati za makubaliano na mikataba au na makubaliano mengine ya kisheria na nyaraka nyingize za kisheria.
  2. Kutoa huduma za kisheria katika mikutano na vikao vya Tume ili Tume iweze kutoa na kufikia maamuzi ya Rufaa na malalamiko ya watumishi wa Umma na kuhakikisha kuwa maamuzi hayo yanajulikana kwa warufani na warufaniwa katika muda unaotakiwa kwa wakati.
  3. Kutoa mwongozo wa kisheria katika vikao vya menejimenti ya Tume, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha na kuelimisha kuhusu masuala ya sheria na utoaji haki kwa watumishi na wadau wa Tume.
  4. Kuainisha na kupendekeza maeneo yanayohitaji kufanyiwa marekebisho/maboresho au kuondolewa katika sheria ya Utumishi wa Umma na kuhakikisha kuwa sheria ya Utumishi wa Umma inatafsiriwa katika Muktadha sawa na sheria nyingine zinazoendana nayo.
  5. Kuratibu mipango na programu za kuwajengea uwezo Makamishna juu ya masuala ya sheria na utoaji wa haki.                                                              
  6. Kushirikiana na kufanya kazi pamoja na mwandishi Mkuu wa Sheria Bungeni (Chief Parliamentary Draftsman) Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (AG &SG) katika kuandaa na kutayarisha miswada ya kisheria/sharia na kanuni za kisheria pamoja na kuwakilisha Serikali katika vyombo vya kutoa haki.
  7. Kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa kesi katika mahakama /mabaraza ya sheria na kutunza kanzidata juu ya maamuzi ya mahakama na rufaa na malalamiko ya Watumishi.
  8. Kutoa ufafanuzi juu ya miongozo inayotolewa, nyaraka, kanuni, hati za makubaliano na nyaraka nyingine za kisheria zinazotolewa nje ya Tume na kutoka katika Idara, Sehemu na Vitengo vilivyopo Tume.
  9. Kuhakikisha kuwa Taasisi za Umma zinazingatia na kutekeleza matakwa ya sheria, kanuni, Taratibu na miongozo ya Utumishi wa Umma iliyopo na kujiridhisha kuwa viwango vilivyowekwa vinafikiwa katika utaratibu mzuri.
  10. Kuhakikisha kuwa, Tume inafuata mfumo halali unaofanya kazi kwa ufanisi, weledi na kwa uwazi katika kutoa maamuzi yake kwa kutoa ushauri sahihi wa kitaalamu katika tasnia ya sheria kwa ujumla.
  11. Kuratibu na kusimamia majukumu ya mamlaka za nidhamu katika kutoa maamuzi kote nchini na kufanya marekebisho au maboresho pale inapobidi kwa lengo la kuhakikisha kuwa sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma zinazingatiwa ipasavyo.