Mipango,Tathmini na Ufuatiliaji
Mipango,Tathmini na Ufuatiliaji
Lengo
Kutoa utaalamu na huduma katika Mipango, Bajeti, Ufuatiliaji na Tathmini katika Tume ya Utumishi wa Umma.
Kitengo kitatekeleza majukumu yafuatayo:
- Kuratibu maandalizi ya Mpango Mkakati wa muda wa kati, Mipango ya Maendeleo na Bajeti ya Tume ikiwemo kufuatilia na kutathmini utekelezaji wake
- Kuandaa Taarifa za vipindi mbalimbali za utekelezaji wa miradi kadri ya muda
- Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Mipango ya Mwaka na Mpango Mkakati wa Muda wa Kati wa Tume
- Kutoa utaalamu na kusaidia michakato ya uandaaji wa Mipango na Bajeti katika Tume
- Kukusanya, kupitia na kuchakata takwimu zinazohitajika katika uandaaji wa mipango na maandiko mbalimbali ya bajeti
- Kuratibu shughuli za utafiti, tathmini ya mipango, miradi na programu zinazofanyika katika Tume
- Kufanya tathmini ya huduma zinazotolewa na Tume kwa wadau
Kitengo kitaongozwa na Mkurugenzi na kitaundwa na Sehemu mbili (2) kama ifuatavyo:
- Sehemu ya Mipango na Bajeti
- Sehemu ya Ufuatiliaji na Tathmini