Miongozo, Uwezeshaji na Utafiti
Miongozo, Uwezeshaji na Utafiti
LENGO
Kutoa miongozo na kufanya utafiti katika Usimamizi wa Rasilimali Watu kwenye eneo la Ajira, Nidhamu, Maendeleo ya Watumishi na Ukaguzi wa Sheria katika Usimamizi wa Utumishi wa Umma.
Kitengo kinatekeleza majukumu yafuatayo-:
- Kuandaa Miongozo ya Ajira, Taratibu za Kushughulikia Mashauri ya Nidhamu, Upandishaji Vyeo, Ukaguzi wa Rasilimali Watu, Upimaji wa Utendaji Kazi, Maendeleo ya Watumishi na Kuandaa taarifa za Utekelezaji wa majukumu ya Kitengo.
- Kutoa ufafanuzi kuhusu Miongozo, Nyaraka, Maelekezo na Kanuni zinazotolewa na Serikali.
- Kuhuisha Miongozo iliyopo na kuisambaza.
- Kutoa elimu kwa Watumishi wa Umma na Wadau wa Tume kuhusu haki zao, wajibu wao na maadili ya Utumishi wa Umma.
- Kuainisha maeneo ya kufanya utafiti na kufanya tafiti mbalimbali kwa ajili ya Utumishi wa Umma ili kuweza kuishauri Serikali kuhusu maeneo hayo.
- Kutoa elimu kwa Waajiri, Mamlaka za Ajira na Nidhamu kuhusu uzingatiaji wa Miongozo inayotolewa na Tume.
- Kuwataarifu Wadau kuhusu mabadiliko ya Miongozo.