Miongozo na Utafiti
Miongozo na Utafiti

Katika eneo la utoaji wa Miongozo, Tume inatoa huduma zifuatazo:-
- Kuandaa Miongozo ya ajira, Mashauri ya Nidhamu, upandishwaji vyeo, ukaguzi wa Rasilimali Watu, upimaji wa utendaji kazi, maendeleo ya watumishi, uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji;
- Kutoa ufafanuzi wa Miongozo, nyaraka, taratibu na maelekezo yanayotolewa/kusambazwa na mamlaka za juu;
- Kufanya maboresho ya Miongozo iliyozalishwa na kusambazwa kwa wadau;Kufanya uwezeshaji kwa watumishi wa umma na wadau kuhusu haki na wajibu, kanuni za maadili na mwenendo katika Utumishi wa Umma;
- Kubainisha maeneo ya kufanya utafiti, kufanya tafiti mbalimbali za Tume, Utumishi wa Umma na kutoa ushauri kutokana na tafiti hizo;
- Kuhamasisha Waajiri, Mamlaka ya ajira na Nidhamu kuhusu uzingatiaji wa Miongozo iliyotolewa;
- Kuandaa na kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa Miongozo iliyoandaliwa na kusambazwa kwa wadau; na
- Kuwafahamisha wadau mabadiliko kuhusu Miongozo ya usimamizi wa rasilimali watu.