Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Watumishi wa Tume wafunzwa Utendaji wa Mfumo wa PSCMIS
09 May, 2025
Watumishi wa Tume wafunzwa Utendaji wa Mfumo wa PSCMIS

  Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw.John C.Mbisso amewataka Watumishi wa Tume kuwa wasikivu katika kujifunza Mfumo wa PSCMIS - Public Service Commission  Management Information Syste

Ameyasema hayo leo Mei 5,2025 katika Ukumbi wa East Africa wa Chuo Kikuuu cha Dodoma wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Mfumo huo wa Kushughulikia Rufaa na Malalamiko ya Watumishi wa Umma kwa Watumishi wa Tume.

Bw.Mbisso amesema kuwa kutokana na Mabadiliko ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Duniani, Tume ya Utumishi wa Umma iliona ni busara kuendana na kasi ya Mabadiliko hayo ili kuboresha Utendaji wa Mtumishi mmoja mmoja na kuweza kutoa huduma kwa wadau katika ubora.

Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Bw.Sylvester Koko amefafanua kuwa Mfumo wa PSCMIS umechakatwa kuanzia Januari 2,2023 na kupitia hatua Sita ambapo hatua ya Saba ni hii ya Mafunzo kwa Watumishi kabla ya kuanza rasmi kutumika.

Ikumbukwe kwamba Mafunzo haya yamewahi kutolewa kwa jumla ya  Maafisa  998 wakiwemo Maafisa TEHAMA  na Maafisa Utumishi kutoka  Taasisi za Umma nchini yaliyofanyika Mkoani Morogoro kuanzia  Februari 10, 2025 mpaka Februari 18, 2025.

Hata hivyo Mafunzo hayo yataendelea kutolewa kadri itakavyoratibiwa ili kusaidia ushughulikiaji wa Rufaa na Malalamiko kuanzia hatua ya upokeaji mpaka utoaji wa maamuzi hali ambayo itarahisisha  usimamizi na utoaji  wa Haki  kwa Wakati.