Karibu PSC

Mhe. Jaji (Mst) Hamisa H. Kalombola
Mwenyekiti
Tume ya Utumishi wa Umma ni chombo rekebu kilichoanzishwa mwaka 2004 chini ya Kifungu cha 9(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298 (Marejeo ya Mwaka 2019) chenye wajibu wa kuhakikisha kuwa Utumishi wa Umma unaendeshwa kwa kuzingatia Sera, Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo.
Kwa mujibu wa Kifungu hicho, Tume ya Utumishi wa Umma inaundwa na Mwenyekiti na Wajumbe sita (6) ambao wote huteuliwa na kuapishwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa sasa, Tume inaongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Mhe. Jaji (Mst) Hamisa H. Kalombola. Wajumbe/ Makamishna ni; Mhe. Balozi John M. Haule, Mhe. Immaculate P. Ngwale, Mhe. Khadija A. M. Mbarak, Mhe. Susan P. Mlawi, Mhe. Balozi Adadi M. Rajabu na Mhe. Nassor N. Mnambila.
Aidha, kwa mujibu wa Kifungu cha 14 cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298, Tume ina sekretarieti ambayo huongozwa na Katibu wa Tume ambaye naye huteuliwa na kuapishwa na Mhe. Rais.