Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Muundo wa Tume ya Utumishi wa Umma


 Kwa mujibu wa Kifungu cha 9(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma , Sura ya 298 kikisomwa kwa pamoja na Aya ya 14(1) ya Taratibu za Uendeshaji za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, Tume ya Utumishi wa Umma inaundwa na Mwenyekiti na Wajumbe Sita ambao wote huteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa sasa Tume inaongozwa na Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Hamisa Hamisi Kalombola (Mwenyekiti) na Wajumbe wa Tume ni hawa wafuatao:- Mhe. Khadija A.M. Mbarak; Mhe. Balozi John M. Haule; Mhe. Immaculata P. Ngwale; Mhe. Balozi Adadi M. Rajabu; Mhe. Nassor N. Mnambila na Mhe.Susan P. Mlawi.

Aidha, kwa mujibu wa Muundo wa Tume ulioidhinishwa mwaka 2018 na Mheshimiwa Rais, Tume ina Idara Tatu (3) na Vitengo Nane (8) ambapo kati ya hizo, Idara 2 na Kitengo 1 zinatekeleza Huduma za Msingi  (Core functions) na Idara 1 na Vitengo 7 zinatekeleza Huduma Saidizi (Supportive functions). 


Organisation Structure .pdf

Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

31-05-2022

TAARIFA KWA UMMA

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.