Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais
Tume ya Utumishi wa Umma
Tume ya Utumishi wa Umma imepewa mamlaka ya kushughulikia Rufaa za
watumishi wa Umma chini ya Kifungu cha 25(1)b cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na.8 ya mwaka 2002 kikisomwa pamoja na Kanuni
ya 60(2) ya Kanuni za Utumishi wa Umma za
mwaka 2003. Mchakato wa Rufaa Tume ya Utumishi wa Umma hupitia katika hatua mbalimbali
zifuatazo:- Tume
kupokea rufaa kutoka kwa watumishi walioadhibiwa na Mamlaka zao za Nidhamu
wakipinga maamuzi yaliyotolewa dhidi yao. Baada
ya kupokea rufaa, Tume huwaandikia Mamlaka za Nidhamu ili walete vielelezo vinavyohusu rufaa
iliyokatwa Tume (muda, vielelezo gani) ndani ya siku kumi na nne (14). Baada
ya kupokea vielelezo kutoka kwa Mamlaka ya Nidhamu, Tume huanza kushughulikia rufaa kwa kufanya uchambuzi wa hoja za
rufaa pamoja na vielelezo vilivyowasilishwa. Rufaa
ikishakamilika kuchambuliwa na Sekretarieti na kuwasilishwa mbele ya Tume kwa
ajili ya maamuzi. Baada
ya maamuzi ya Tume, watumishi waliokata rufaa Tume hujulishwa uamuzi wa rufaa
zao kwa barua.
Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.