Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais
Tume ya Utumishi wa Umma
UTANGULIZI Tume ya Utumishi wa Umma hufanya
ukaguzi wa Rasilimali Watu kwa kutumia Mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha
10 (1) (c) cha Sheria Na.18 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na.
18 ya mwaka 2007, sheria hii imepatia mamlaka Tume kusimamia Waajiri, Mamlaka
za Ajira na Nidhamu kuhakikisha kuwa wanazingatia ipasavyo Sheria, Kanuni na
Taratibu katika kusimamia Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma. Kwa mujibu wa Sheria hiyo, Tume ya
Utumishi wa Umma ina mamlaka ya kufanya ukaguzi wa uzingatiaji wa Rasilimali
Watu katika taasisi zote za umma nchini ikiwemo Wizara, Idara Zinazojitegemea,
Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wakala za Serikali na
Taasisi za Umma. Tume hufanya ukaguzi kwa kutumia
mfumo wa ukaguzi wa Uzingatiaji wa Rasilimali Watu wa Tume unaoitwa “Human
Resource Compliance Inspection System” (HRCIS) ulioanzishwa mwaka 2005. Mfumo
huu umeandaliwa ili kuiwezesha Tume kufanya tathmini ya uzingatiaji katika maeneo ya
Ajira, Likizo ya mwaka, Nidhamu, OPRAS, Likizo ya ugonjwa, Upandishwaji
vyeo na Usimamizi wa mafunzo.
Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.