Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Majukumu na Mamlaka ya Tume


MAJUKUMU YA TUME YA UTUMISHI WA UMMA

Kifungu cha 10(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 kimeainisha majukumu ya Tume kama ifuatavyo:-

i) Kumshauri Rais kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma katika kutekeleza majukumu yake aliyopewa Kikatiba chini ya Ibara ya 36 kuhusu ujazaji wa nafasi wazi katika Utumishi wa Umma kadri atakavyohitaji;

ii) Kumsaidia Rais kuhusu masuala mbalimbali ya kiutumishi kadri atakavyohitaji;

iii) Kutoa Miongozo na kufuatilia Uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu katika Utumishi wa umma;

iv) Kupokea na kushughulikia rufaa za mashauri yaliyotolewa uamuzi na Mamlaka za Nidhamu;

v) Kuwezesha,kufuatilia na kutathmini utendaji kazi wa Watumishi wa Umma wa ngazi mbalimbali ili uwe na ufanisi na wenye kuzingatia matokeo; na

vi) kuhakikisha kuwa Taratibu za Uendeshaji za Utumishi wa makundi mbalimbali ya kiutumishi zinatayarishwa na kutumika ipasavyo.

MAMLAKA YA TUME YA UTUMISHI WA UMMA

Mamlaka ya Tume yameainishwa katika Kifungu cha 10(1)(2) cha Sheria tajwa hapa juu ambayo ni:-

i) Kuwaita Watendaji Wakuu kutoa maelezo kuhusu utendaji kazi usioridhisha pale Tume inapokuwa na ushahidi au malalamiko yanayohusu ukiukwaji wa Sheria, kanuni na taratibu;

ii) Kuchukua hatua kupitia Mamlaka zao za Nidhamu Watendaji Wakuu watakaoshindwa kuwachukulia hatua watumishi walio chini yao wenye utendaji usioridhisha kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu; na

iii) Kuzitaka Mamlaka za Ajira kuwasilisha taarifa ambazo tume itazihitaji kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake.


 
 

MAJUKUMU YA TUME.pdf

Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

31-05-2022

TAARIFA KWA UMMA

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.