Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Katibu wa Tume Bw. Nyakimura Muhoji (kulia) akifafanua kuhusu jukumu la Urekebu la Tume katika kushughulikia rufaa na malalamiko ya watumishi wa Umma. Kushoto ni Katibu Msaidizi wa Tume Bw. Peleleja Masesa. M/kiti wa Tume ya Utumishi wa Umma (Jaji Mstaafu) Dkt. Steven Bwana (mbele katikati) akizungumza katika kikao cha pamoja na Maafisa kutoka UNDP - Tanzania Bw. David Omozuafoh na Bi Natalie Rolloda (kulia) walipotembelea ofisi za Tume. Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Nyakimura Muhoji (kulia) akifuatilia mada wakati wa mjadala kwenye maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa, uliofanyika Jijini Dodoma. Washiriki wakifuatilia mada wakati wa mjadala kwenye maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa, uliofanyika Jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Tume Bibi Mery Fidelis. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa  (Mb) akizungumza na watumishi wa Umma na wananchi wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya Mwl. Nyerere Square. Naibu Waziri, Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa na Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma mara baada ya kufungua mafunzo elekezi ya Makamishna hao, Dar es sallam. Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma (Jaji Mstaafu) Dkt. Steven Bwana akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) katika ufunguzi wa mafunzo elekezi ya Makamishna Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Asifiwe Kyando (aliyesimama) akielezea changamoto zinazoukabili Utumishi wa Umma katika kikao na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa. Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Richard Odongo (kulia) akielezea majukumu ya Tume kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa alipotembelea ofisi za Tume na kuzungumza na watumishi Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akiangalia vielelezo vya watumishi wa Taasisi za Umma waliokata rufaa katika Tume ya Utumishi wa Umma alipotembelea ofisi za Tume. Waziri wa UTUMISHI na Utawala Bora Kapt. (Mstaafu) Mhe. George Mkuchika (katikati) akiwa na Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma baada ya kufanya nao kikao katika ofisi za Tume Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Kaimu Katibu wa Tume Bw. Richard Odongo Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Litson Magawa (aliyesimama) akizungumza katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Umma lililofanyika katika ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma (Jaji Mstaafu) Dkt. Steven Bwana (aliyesimama) akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Umma lililofanyika katika ofisi ya Tume Jijini Dar es Salaam.

Karibu Tume ya Utumishi wa Umma

 

Tume ya Utumishi wa Umma imeundwa chini ya Kifungu Na. 9(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298. Tume ilianza kufanya kazi rasmi tarehe 7/1/2004 baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuteua viongozi ( Mwenyekiti, Makamishna na Katibu wa Tume) kusimamia utendaji wake.

Kazi kubwa ya Tume ya Utumishi wa Umma ni kufuatilia na kusimamia uendeshaji wa shughuli za Rasilimali watu katika Taasisi za Umma na kuhakikisha kuwa Utumishi wa Umma unaendeshwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu.

Tume ya Utumishi wa Umma inaendelea kushirikiana na wadau wake wote ili kuhakikisha kuwa U...

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.