Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Maswali yaulizwayo Mara kwa Mara

Tume ya Utumishi wa Umma imekuwa ikilaumiwa kwa kuchelewesha kutoa uamuzi wa rufaa zinazowasilishwa mbele yake, sababu ni nini?

Tume inatakiwa kuamua rufaa ya mtumishi ndani ya Siku 90 tangu kupokelewa kwa rufaa husika kama kila mdau ametimiza wajibu wake. Ucheleweshaji wa kuamua rufaa unaweza kusababishwa na Mamlaka ya Nidhamu kuchelewesha kuwasilisha vielelezo Tume. Ili haki ya msingi kati ya mrufani na mrufaniwa ni lazima vielelezo vyote viwepo ili kuweza kutoa uamuzi wa haki.

Nini Wajibu wa Mtumishi anayewasilisha rufaa Tume ya Utumishi wa Umma?.

Wajibu wa Mtumishi ni kujua haki yake ili isipotee pale ambapo anaona hajatendewa haki katika masuala yake ya kiutumishi na kuwasilisha Rufaa yake kwa Mamlaka husika kwa muda uliowekwa Kisheria. Mtumishi anatakiwa kuwasilisha Rufaa Tume ndani ya muda usiozidi siku 45 tangu alipopokea barua ya uamuzi kutoka katika Mamlaka ya Nidhamu. (Kwa mujibu wa Kanuni ya 61 (1) ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003). Aidha, hata masuala ya malalamiko yana muda maalum wa kuwasilishwa Tume, kwa mujibu wa Kanuni Q. 19 ya Kanuni za Kudumu za utumishi wa umma za mwaka 2009 anatakiwa awasilishe ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

Nini Wajibu wa Mamlaka ya Nidhamu kwa Tume ya Utumishi wa Umma?.

Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Kanuni zake Mamlaka ya Nidhamu ina wajibu wa kuwasilisha Vielelezo vyote vilivyotumika katika mchakato wa kumchukulia hatua za nidhamu Mtumishi hadi pale uamuzi unapotolewa. Kwa mujibu wa Kanuni 61 (3) iko wazi kwamba, pale Mamlaka ya Nidhamu imepata nakala kutoka kwa mrufani ama Mamlaka ya Rufaa ndani ya siku 14 inatakiwa iwasilishe vielelezo kwa Mamlaka ya Rufaa. Tume ya Utumishi wa Umma imepewa Mamlaka za kuwataka Waajiri wawasilishe taarifa zote ambazo Tume itazihitaji kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake.

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.