Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Tume huchukua hatua gani dhidi ya Waajiri, Mamlaka za Ajira na Mamlaka za Nidhamu pale ambapo hazitekelezi maagizo yake?

Kifungu cha 10(1) (g) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298 [Marejeo ya mwaka 2019] kinaipa Tume mamlaka ya kuwaita Watendaji Wakuu katika Utumishi wa Umma kufika mbele yake kujieleza inapokuwa na ushahidi wa Watendaji hao kushindwa kutekeleza maagizo/uamuzi wa Tume.

 Tume isiporidhika na maelezo yao huchukua hatua kwa kuzitaarifu Mamlaka za       Nidhamu    za Watendaji hao ili hatua zaidi zichukuliwe