Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Tofauti ya Ukaguzi wa Kawaida na Ukaguzi Maalum wa Uzingatiaji wa Sheria katika Usimamizi wa Masuala ya Rasilimali Watu.

i) Ukaguzi wa Kawaida

Hufanyika kila baada ya mwaka wa fedha kukamilika kwa lengo la kuangalia Uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu kwenye michakato mbalimbali ya masuala ya Kiutumishi. Ukaguzi huu umelenga kuangalia masuala ya kiutumishi yaliyotengewa fedha katika mwaka wa fedha husika kama yametekelezwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu na watumishi wamepata stahili zao.

 

ii) Ukaguzi Maalum

Ukaguzi maalum hufanyika kufuatia maelekezo ya Serikali yakiwemo ya Katibu Mkuu Kiongozi, Katibu Mkuu UTUMISHI; na maelekezo ya Tume yenyewe kutokana na upungufu au kasoro zilizobainika kwenye Taasisi za Umma wakati wa ukaguzi wa kawaida na kasoro zinazoweza kubainika wakati wa kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa watumishi. Aidha, Taasisi yenyewe inaweza kuiomba Tume kufanya ukaguzi kwa lengo la kubainisha upungufu unaohitaji kufanyiwa kazi katika Taasisi zao.