Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Ni uamuzi gani ambao Tume inaweza kuutoa katika kushughulikia rufaa?

Kwa mujibu wa Kanuni ya 60 (1) ya Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2022 Tume inaweza ikatoa uamuzi ufuatao:-

  • Kukubali rufaa bila masharti: 

Pale ambapo tuhuma dhidi ya mrufani hazijathibitika na mchakato wa masuala ya nidhamu ulifuata taratibu zote. 

Kwa uamuzi huu Mtumishi anarejeshwa kazini na kulipwa haki/stahiki zake zote.

 

  • Kukubali rufaa kwa masharti:  

Ni pale ambapo mchakato wa masuala ya nidhamu haukuzingatia haki za msingi za mtumishi mtuhumiwa. 

Tume huagiza shauri lianze upya kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu.

Tume inaweza pia kukubali rufaa kwa sharti la kupunguza adhabu aliyopewa mtumishi baada ya kuangalia uzito wa kosa lililotendeka na misingi ya kufikia uamuzi.

  • Kukataa rufaa:

Hutokea pale ambapo tuhuma zimethibitika na mchakato wa masuala ya nidhamu ulifuata taratibu zote.

Kwa uamuzi huu, adhabu aliyopewa Mtumishi na Mamlaka yake ya Nidhamu inathibitishwa na Tume.

 

  • Rufaa kutupiliwa mbali:

Hutokea pale ambapo rufaa au lalamiko limewasilishwa Tume nje ya muda uliowekwa Kisheria bila sababu za msingi au bila mrufani kutoa sababu yoyote ya kuwasilisha nje ya muda unaotakiwa.