Misingi ipi Tume inatumia katika kuamua rufaa zinazowasilishwa mbele yake
Misingi ipi Tume inatumia katika kuamua rufaa zinazowasilishwa mbele yake
Kifungu cha 23 cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298 (Marejeo ya mwaka 2019) kimeainisha mambo matatu muhimu ya kuzingatia wakati wa kushughulikia mashauri ya nidhamu kwa watumishi wa umma. Misingi hiyo ndiyo inayoangaliwa na Tume kama mamlaka ya Nidhamu imeizingatia. Misingi hiyo ni:-
- Mtumishi mtuhumiwa kupewa Hati ya Mashtaka na Notisi
- Mtumishi mtuhumiwa kupewa fursa ya kusikilizwa na Kujitetea
- Kuundwa kwa Kamati ya Uchunguzi wa shauri endapo mtumishi mtuhumiwa atakana kosa