Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Salamu za rambi rambi za Tume - kufuatia kifo cha Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania, Alhaj Ali Hassan Mwinyi

Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji mstaafu mheshimiwa Hamisa Hamis Kalombola  ametuma salamu za rambi rambi kufuatia kifo cha Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania, Alhaj Ali Hassan Mwinyi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Tume iliyotolewa leo Jijini Dodoma na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Mheshimiwa Jaji mstaafu Kalombola amesema kuwa Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Umma imepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa kifo cha Rais wa Awamu ya pili, Hayati Ali Hassan Mwinyi, kilichotokea tarehe 29 Februari 2024 katika Hospitali ya Mzena, jijini Dar-es-Salaam.

 

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.