Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi wa Ubora wa Ujenzi wa Majengo ya Serikali Jijini Dodoma, yatembelea mradi wa Ujenzi wa Jengo la Tume- Mtumba Dodoma

Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Ubora wa Ujenzi wa Majengo ya Serikali Jijini Dodoma QS. Dkt. Godwin Maro na Wajumbe wa Kamati kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 10 Januari 2024  watafanya ziara kutembelea mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma linalojengwa katika mji wa Serikali Mtumba, Dodoma. Katika ziara hii watakagua hatua iliyofikiwa katika ujenzi, kuangalia muundo wa jengo, vifaa na huduma. Kamati itakutana na Kaimu Katibu wa Tume Bw. Charles Mulamula, Menejimenti ya Tume, Mkandarasi CRJE na Mtaalam Mwelekezi TBA. 

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.