Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Serikali yasisitiza Uzingatiaji wa Sheria
10 Sep, 2026
Serikali yasisitiza Uzingatiaji wa Sheria

 

Serikali imesisitiza umuhimu wa watumishi wa umma kuzingatia Sheria, Sera, Kanuni, Taratibu, Miongozo na Maadili ya Utumishi wa Umma ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

 

Hayo yamesemwa leo Septemba 7, 2026 jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (Mb), wakati alipotembelea Bodi ya Usajili wa Wahandisi kukagua utekelezaji wa zoezi la Ukaguzi wa Uzingatiaji wa Sheria katika Usimamizi wa Utumishi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

 

Mhe. Qwaray amesema ukaguzi huo unaofanywa na Tume ya Utumishi wa Umma ni muhimu kwa Serikali kupata taarifa kuhusu hali ya uzingatiaji wa sheria katika usimamizi wa masuala ya kiutumishi, pamoja na kubaini maeneo yanayohitaji maboresho ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati.

 

Amesema taarifa zinazotokana na ukaguzi huo huisaidia Serikali kufanya maamuzi na kupanga mipango ya rasilimali watu kwa kuzingatia ushahidi, huku pia zikitoa mrejesho kuhusu utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma na kusaidia kuweka ulinganifu katika tafsiri na utekelezaji wake.

 

Aidha, ameipongeza Tume ya Utumishi wa Umma kwa kuanzisha Mfumo wa Kielektroniki wa Ukaguzi wa Uzingatiaji wa Sheria katika Usimamizi wa Utumishi wa Umma, akieleza kuwa matumizi ya mfumo huo yanaendana na jitihada za Serikali za kutumia TEHAMA katika kuboresha utendaji na usimamizi wa shughuli za Serikali.

 

Ameeleza kuwa Serikali imeendelea kujenga mifumo mbalimbali ikiwemo e-Watumishi na e-Utendaji kwa lengo la kuongeza ufanisi katika usimamizi wa watumishi wa umma.

 

Katika hatua nyingine, Mhe. Qwaray amewataka watumishi na wasimamizi kuzingatia maelekezo ya utekelezaji wa PEPMIS, akibainisha kuwa changamoto ya baadhi ya watumishi kushindwa kufikia asilimia 75 zinazohitajika katika mchakato wa kupandishwa vyeo inaweza kuchangiwa na kutokuzingatiwa ipasavyo kwa majukumu na taratibu za mfumo huo.

slot gacor