Tume yaikagua TISEZA
Tume yaikagua TISEZA
14 Sep, 2026
12:30PM - 01:PM
DODOMA
-
Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi (TISEZA) imefanya kikao na timu ya Tume ya Utumishi wa Umma, kilichoongozwa na Mh. Adadi Mohamed Rajabu, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma.
Kikao hicho kililenga kufungua rasmi ukaguzi wa masuala ya kiutumishi, kwa kuangazia maeneo 11 muhimu yanayolenga kuimarisha utendaji, uwajibikaji na ufanisi katika kutekeleza majukumu ya watumishi wa umma.
Hatua hii ni sehemu ya kuhakikisha mifumo ya utumishi inaimarishwa na watumishi wanatekeleza wajibu wao kwa ufanisi, weledi na kwa kuzingatia viwango vinavyotarajiwa katika utumishi wa umma.