TUME YA UTUMISHI WA UMMA YAFANYA BARAZA LA WAFANYAKAZI
Tume ya Utumishi wa Umma imefanya kikao cha Baraza la Wafanyakazi leo Novemba 5, 2026 katika Ukumbi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi Jijini Dodoma, kwa lengo la kupitia na kutathmini utekelezaji wa Bajeti ya Tume kwa mwaka wa fedha 2025/2026, pamoja na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa majukumu na shughuli za Tume.
Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mheshimiwa Jaji (mst.) Hamisa H. Kalombola, amesisitiza kuwa milango yake pamoja na ile ya Makamishna iko wazi kwa Menejimenti pale inapokabiliwa na changamoto katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Tume.
Amesema kuwa atakuwa tayari kutumia uzoefu na busara zake, kwa kushirikiana na Makamishna, katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto zitakazojitokeza ili kuhakikisha shughuli za Tume zinatekelezwa kwa ufanisi na kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Aidha, amehimiza ushirikiano na mawasiliano ya wazi kati ya uongozi na Menejimenti ili kurahisisha utatuzi wa changamoto na kuimarisha utekelezaji wa majukumu.