Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Mtumishi wa Umma anategemea kupata nini anapoleta suala lake Tume ya Utumishi wa Umma?

Mtumishi wa Umma anapowasilsha Rufaa yake Tume atarajie mambo mawili ambayo ni kukubaliwa au kakataliwa kwa rufaa yake.

1. Rufaa kukubaliwa:

Kuna aina mbili za kukubaliwakwa rufaa ya Mtumishi  wa Umma ambazo ni :-

  • Kukubaliwa bila masharti ni pale ambapo tuhuma dhidi ya mrufani hazijathibitika na mchakato wa masuala ya nidhamu ulifuata taratibu zote. Kwa hiyo, uamuzi wa Tume unakuwa , Rufaa ya Mtumishi wa Umma imekubaliwa arejeshwe kazini na kulipwa haki zake zote au apewe tuzo kulingana na adhabu aliyopewa.
  • Kukubaliwa kwa masharti ni pale ambapo tuhuma dhidi ya mrufani hazikuthibitika ama mchakato wa masuala ya nidhamu haukuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu. Kwa mujibu wa Kanuni ya 62(3) ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2022.

2. Rufaa kukataliwa:

Rufaa ikikataliwa ni pale ambapo tuhuma zimethibitika na mchakato wa masuala ya nidhamu ulifuata taratibu zote. Uamuzi wa Tume ni kwamba Rufaa imekataliwa na Tume imethibitisha adhabu aliyopewa mrufani ni Mamlaka yake ya Nidhamu.