Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Bw. Elikana Balandya, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza amefungua Kikao Kazi cha Tume na watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Elikana Balandya amefungua Kikao kazi kati ya Tume ya Utumishi wa Umma na watumishi wa umma kutoka Mamlaka ya Serikali za Mitaa. Lengo la kikao hiki ni kuwajengea uwezo watumishi wa kuzielewa, kutafsiri na kusimamia Sheria, Kanuni na Taratibu zinazoongoza Utumishi wa Umma kwa lengo la kuhakikisha kwamba Utumishi wa Umma katika ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa unazingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma.  Washiriki katika kikao hiki wanatoka Kanda ya Ziwa ambao ni Waheshimiwa Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Idara za Utawala na Utumishi na Wanasheria na Watumishi wa Umma.

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.