Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais
Tume ya Utumishi wa Umma
Tume ya Utumishi wa Umma ni miongoni mwa Taasisi za Umma (55) zilizoshiriki katika hafla ya kukabidhi vibali vya ujenzi wa Ofisi za Taasisi, Dodoma iliyofanyika Ukumbi wa Hazina, Dodoma. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George B. Simbachawene (Mb) amemkabidhi kibali cha ujenzi wa Ofisi ya Tume inayojengwa katika Mji wa Serikali Mtumba Bw. Mathew M. Kirama, Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma na katika hotuba yake Mhe. Waziri Simbachawene ( Mb) amemshukuru Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendeleza dhamira yake ya dhati ya kuhakikisha anatekeleza kwa umadhubuti mkubwa Mpango wa muda mrefu wa kuhamishia shughuli za Serikali katika Makao Makuu ya Nchi Jijini Dodoma.
Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.