Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Wataalam wa Tume waketi kupitia Miongozo ya ndani na kuiboresha
29 Jan, 2025
Wataalam wa  Tume waketi kupitia Miongozo ya ndani na kuiboresha

                                

   Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. John C. Mbisso amefungua Kikao kazi cha kupitia Miongozo ya ndani ya Tume ya Utumishi wa Umma kilichoratibiwa na Kitengo cha Miongozo, uwezeshaji na Utafiti na kufanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Veta Jijini Dodoma  Januari 27,2025.

Bw.Mbisso amesisitiza ushiriki mzuri wa Washiriki wa Kikao kazi hicho ambao ni Maafisa kutoka Idara na Vitengo mbalimbali vya Tume,  ili kufikia Malengo yaliyokusudiwa ya kukamilisha maboresho ya Miongozo ya ndani inayotolewa na Tume ambayo italeta tija kwa Maafisa Wachambuzi wa Rufaa na Wakaguzi wa Rasilimali Watu.

“Kikao kazi hiki kinafanyika ili kutekeleza moja ya majukumu ya kisheria ya Tume kama yaliyoainishwa chini ya kifungu cha 10 (1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298 ( Marejeo ya mwaka 2019) jukumu la kutoa Miongozo na kufatilia uzingatiaji wa Sheria , Kanuni na Taratibu katika Utumishi wa Umma” alisema Mbisso.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Miongozo, Uwezeshaji na Utafiti  Bw. Peleleja Masesa ameeleza kuwa Kikao kazi hicho ni utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa katika Mkutano wa Tume NO.3 wa mwaka 2022/2023 na uzingatiaji wa Maoni kutoka  Taasisi simamizi za Utumishi wa Umma kama TAMISEMI, Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) na nyinginezo zilizotoa maoni kupitia kikao kazi kilichofanyika Morogoro 17 – 19 Oktoba 2022 hivyo ni wakati muafaka sasa wa kutekeleza agizo hilo kwa kupitia kwa umakini maoni yaliyotolewa na kuboresha kabla ya kuwasilishwa kwenye Menejimenti  ya Tume ili iweze kutumika.

Miongozo inayopitiwa na kuboreshwa ni Mwongozo wa Uchambuzi wa Rufaa na Malalamiko na Mwongozo wa Ukaguzi wa Uzingatiaji wa Rasilimali