Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Tume yafanya Mkutano wake wa Tatu 2024/2025
17 Apr, 2025
Tume yafanya Mkutano wake wa Tatu 2024/2025

  Tume ya Utumishi wa Umma imefanya Mkutano wake Na. 3 kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 kuanzia tarehe 03/03/2025 hadi 21/03/2025 chini ya Mwenyekiti wake Jaji (Mst.) Hamisa H. Kalombola ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Tume za Utumishi wa Umma Afrika (AAPSCOMS), Kanda ya Afrika Mashariki. Mkutano huo hufanyika kutokana na  Mamlaka Tume iliyonayo chini ya Vifungu vya 10(1) na 25(1)(b) vya SheriKutokana na  Mamlaka Tume iliyonayo chini ya Vifungu vya 10(1) na 25(1)(b) vya Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298 (Marejeo ya Mwaka 2019).

Katika Mkutano huo, Tume imetekeleza majukumu mbalimbali ambapo kuanzia tarehe 03/03/2025 hadi 06/03/2025, Tume imefanya Ziara ya kujifunza pamoja na kutoa elimu ya masuala ya Kiutumishi katika Taasisi za Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Shirika la Reli Tanzania (TRC), Jijini Dar es Salaam.

Aidha, kuanzia tarehe 10/03/2025 hadi 21/03/2025, Tume imepitia, kujadili na kuamua Rufaa 62 na Malalamiko 25 ya Watumishi wa Umma yaliyowasilishwa mbele yake kwenye Ukumbi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) katika Jiji la Dodoma.