Kamati ya Ukaguzi yazinduliwa.

Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Bw. Umma John C. Mbisso amezindua Kamati ya Ukaguzi ya Tume ya Utumishi wa Umma Januari 22,2025 katika Ukumbi wa Posta - B Jijini Dodoma. Kamati itakuwa na Jukumu la kutoa ushauri kuhusiana na Usimamizi juu ya Matumizi sahihi ya Rasilimali za Umma, Utawala bora na masuala ya vihatarishi.
Bw.Mbisso amewapongeza Wajumbe wa Kamati hiyo kwa kuaminiwa na kuteuliwa kwa kubainisha kuwa yapo mabadiliko yaliyofanyika katika upatikanaji wao kutokana na Mabadiliko ya Kanuni za Sheria ya Fedha ( Sura ya 348) ya Mwaka 2024 ambapo Wajumbe wote wanatakiwa kutoka nje ya Taasisi tofauti na hapo awali.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Salim A. Masha ameahidi kusimamia Kanuni hiyo katika utekelezaji wa Majukumu yake akishirikiana na Katibu wa Kamati pamoja na Wajumbe na kuhakikisha kuwa Afisa Masuhuli wa Tume ya Utumishi wa Umma anafanikiwa katika utendaji wa kazi zake.
Wajumbe wa Kamati ya Ukaguzi wamepata wasaa wa kufahamau utendaji Kazi wa Tume ya Utumishi wa Umma kupitia Mawasilisho mbalimbali yaliyotolewa na Wataalam kutoka Idara na Vitengo vya Tume ya Utumishi wa Umma.