Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa 2019 kufanyika Dodoma

Wakuu wa Taasisi Simamizi za masuala ya Maadili na Utawala Bora, zinazoratibu kwa pamoja Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa tarehe 10 Disemba 2019 wamefanya kikao cha maandalizi ya Maadhimisho hayo jana jijini Dodoma. Taasisi hizo ni Ofisi ya Rais- Ikulu; Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma; Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora; Tume ya Utumishi wa Umma; Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma; Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali; Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa; Wizara ya Katiba na Sheria na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Kauli Mbiu ya Maadhimisho kwa mwaka 2019 ni:- MAADILI KATIKA UTUMISHI WA UMMA NI NGUZO MUHIMU KATIKA KUIMARISHA UTAWALA BORA NA HAKI ZA BINADAMU.

Pichani: MHESHIMIWA Jaji (Mstaafu) Harold R. Nsekela, Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma, akifafanua jambo wakati wa Kikao cha maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Maadili Kitaifa kilichofanyika 29/11/2019  jijini Dodoma. Kulia ni Bwana Nyakimura Muhoji, Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma.   

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.