Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Madiwani epukeni mgongano wa maslahi tendeni haki mnapotoa uamuzi kwa Watumishi wa Umma

MWENYEKITI wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Dkt. Steven James Bwana amewataka Madiwani kuepuka mgongano wa maslahi na pia watende haki wanapotoa uamuzi katika mashauri ya nidhamu kwa watumishi wa umma.

Mheshimiwa Dkt. Bwana amesema kupitia rufaa na malalamiko yanayowasilishwa,  Tume imebaini kuwa baadhi ya Mamlaka za Nidhamu (Baraza la Madiwani) katika Halmashauri zimekuwa na misimamo yenye mgongano wa maslahi kunakosababisha ukiukwaji wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo wakati wa kutoa uamuzi wa mashauri yanayowakabili watumishi wa umma.

 

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.