Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma wametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Tume, Mji wa Serikali Mtumba- Dodoma

Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma wametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Tume, Mji wa Serikali Mtumba- Dodoma. Akizungumza wakati wa ziara hiyo iliyolenga kuangalia hatua ya ujenzi iliyofikiwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji (mstaafu) Mhe. Hamisa H. Kalombola amesema ni muhimu kwa Kampuni iliyopewa kazi ya CRJE kuhakikisha inafanya kazi kwa viwango vya ubora pamoja na thamani ya fedha, pamoja na kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati. Amesisitiza Mwelekezi wa Ujenzi (TBA) kuhakikisha wanabaini changamoto zinazoweza kukwamisha ili zipatiwe ufumbuzi. kwa upande wake Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Mathew M. Kirama amesema hadi sasa mradi unaendelea vizuri na matarajio ni kuwa utakamilika kwa wakati. 

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.