Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Hali ya uzingatiaji wa Sheria katika Mamlaka za Serilali za Mitaa si nzuri.Tume inachukua hatua zipi?

Tume ina jukumu la kuwezesha Taasisi za Umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2004, Tume imekuwa ikifanya uwezeshaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ingawa haijaweza kuzifikia Mamlaka zote kutokana na changamoto ya Rasilimali zilizopo.

Tume inafahamu kuwa kumekuwepo na mabadiliko ya mara kwa mara ya baadhi ya Viongozi na watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini, pamoja na marekebisho ya Sheria, Kanuni na Taratibu zinazosimamia masuala ya Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma. Tume inaandaa mikakati ya namna ya kufanya uwezeshaji katika masuala ya uzingatiaji wa usimamizi wa Rasilimali watu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na hatimae kufikia malengo ya Serikali.