Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Tume ya Utumishi wa Umma inajuaje kama tuhuma dhidi ya mrufani imethibitika?

Tume kama cbombo cha kutoa haki inapoamua rufaa inapitia vielelezo vyote kutoka katika Mamlaka ya Nidhamu kuangalia jinsi mchakato ulivyofanyika. Kamati ya Uchunguzi ndicho chombo ambacho kwa mujibu wa Sheria kimepewa wajibu wa kuthibitisha kama tuhuma zilizopo katika hati ya mashtaka na utetezi wa mtumishi mtuhumiwa zimethibitika ama hazijathibitika.

Hivyo Tume hutoa uamuzi wake baada ya kupitia vielelezo vilivyowasilishwa  ikiwemo hoja za mrufani anazowasilisha kupinga uamuzi uliotolewa na Mamlaka yake ya Nidhamu na taarifa ya Kamati ya Uchunguzi yenye jukumu la kuthibitisha tuhuma dhidi ya mrufani.