Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Mkutano wa Tume Umeanza leo tarehe 15 Machi 2021 Jijini Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma mheshimiwa Jaji (mst) Dk. Steven J. Bwana leo tarehe 15 Machi 2021 ameongoza Mkutano wa Tatu wa Tume kwa mw aka wa fedha 2020/2021 unaofanyika Jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huu, rufaa na malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa Tume na watumishi wa umma ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa na Waajiri, Mamlaka za Ajira na Nidhamu katika Utumishi wa Umma yatatolewa uamuzi. Mkutano huu unahudhuriwa na Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma pamoja na Sekretarieti ya Tume. 

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.