Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais
Tume ya Utumishi wa Umma
Tume ya Utumishi wa Umma inafanya Ukaguzi wa Rasilimali watu kwenye Taasisi 30 katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Katika Mpango Kazi wa Tume kwa mwaka wa fedha 2020/2021, imepanga kufanya Ukaguzi wa Rasilimali Watu katika Taasisi za Umma 160. Kwa mujibu wa marekebisho ya Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298, kuna Taasisi za Umma mpya zimejumuishwa na zitakaguliwa na Tume kuhusu masuala ya Rasilimali Watu. Lengo la Tume ni kuzifikia Taasisi zote na katika Awamu ya Pili, Tume imepanga kuzikagua Taasisi zilizopo Jijini Dodoma.
Tume ya Utumishi wa Umma (PSC) hufanya Ukaguzi wa Rasilimali Watu katika Taasisi za Umma kwa lengo la kubaini kiwango cha uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu kwa Waajiri, Mamlaka za Ajira na Mamlaka za Nidhamu. Ukaguzi huu pia, husaidia kupunguza malalamiko ya Watumishi wa Umma.
Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.