Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, 16-23 JUNI 2020

Tume ya Utumishi wa Umma inapenda kuwajulisha watumishi wa umma na wananchi wote kuwa kuanzia leo tarehe 16 hadi 23 Juni 2020,  itakuwa inapokea na kusikiliza kero na malalamiko ya watumishi wa umma kuhusu masuala mbalimbali ya kiutumishi. Hii ni katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma.

Tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona inapewa kipaumbele katika kipindi hiki. Tunatakiwa kuzingatia Miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya pamoja na maelekezo ya Viongozi Wakuu wa Nchi. Aidha,  watumishi wa umma na wananchi wote wanataarifiwa kuwa wanaweza kuwasilisha kero na malalamiko yao kwa kutuma kwa barua pepe kwa anuani ya secretary@psc.go.tz au kupiga simu namba 0738 166 703.

Kupitia maadhimisho haya Tume inawakumbusha Waajiri, Mamlaka za Ajira, Mamlaka za Nidhamu pamoja na Watumishi wa Umma kuhakikisha wakati wote wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu, Miongozo na Maelekezo halali yanayotolewa na Serikali.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2020 ni: “Jukumu la Utumishi wa Umma katika Kujenga na Kudumisha Amani iliyopo Miongoni mwa Jamii”.
  

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.