Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

JAJI MSTAAFU MHE. DKT. STEVEN JAMES BWANA AMEMUAPISHA BW. MUSSA MAGUNGULI KUWA KAIMU 'DPM&E'- TUME YA UTUMISHI WA UMMA

Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, mheshimiwa Jaji (mstaafu)  Dkt. Steven James Bwana leo tarehe 25 Machi 2020, amemuapisha ndugu Mussa Magunguli kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini katika Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Umma. Tukio hili limehudhuriwa pia na bwana John Mbisso, Kaimu Katibu wa Tume, Bibi Eliaika Manyanga, Mkurugenzi Msaidizi (Utawala), bwana Charles Mulamula, Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria na bwana Richard Cheyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.  Hafla fupi  ya kumuapisha bwana Magunguli imefanyika leo katika Ofisi ya Tume, jijini Dar es Salaam.   

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.