Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Mkuchika kuongoza Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu leo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Kapt. (Mstaafu) George H. Mkuchika (Mb), leo tarehe 11 Disemba 2019 anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, yanayofanyika Kitaifa jijini Dodoma.
Maadhimisho haya yatafanyika kwa kuwakutanisha watumishi wa Umma katika Kongamano linalofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Ofisi ya Bunge jijini Dodoma. Miongoni mwa waalikwa katika Kongamano hili la Maadhimisho haya ni baadhi ya Viongozi wakuu wastaafu, Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali, baadhi ya Wawakilishi wa Jumuiya za Kimataifa na watumishi wa Umma.
 

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.