Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi wa Umma

Mkutano wa Tatu wa Tume kwa mwaka 2023/2024 umehitimishwa leo tarehe 08 Machi 2024 Jijini Dodoma

Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Mhe. Jaji (Mst.) Hamisa Hamis Kalombola pamoja na Makamishna wa Tume, leo tarehe 08 Machi 2024 wamehitimisha Mkutano wa Tume wa Tatu kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
 Mkutano wa Tume umefanyika  kuanzia tarehe 19 Februari, 2024 hadi 08 Machi, 2024 Jijini Dodoma.
Katika Mkutano huo, jumla ya Rufaa na Malalamiko 342 yaliwasilishwa na kutolewa uamuzi katika mchanganuo ufuatao:-
(i) Rufaa 160 zilisikilizwa na kutolewa uamuzi, na
(ii) Malalamiko 182 yalisikilizwa na kutolewa uamuzi. 
Aidha, kwa mujibu wa Kanuni ya 62(1) ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2022, Warufani 21 na Mrufaniwa mmoja (01) walitumia haki yao ya kisheria kufika  mbele ya Tume na kutoa ufafanuzi wa hoja zao za rufaa na malalamiko.
Katika Mkutano huo wa Tatu wa Mwaka 2023/2024, makosa yaliyoonekana kutendwa zaidi ni pamoja na; utoro kazini, kuajiriwa bila kuwa na sifa, kukiuka Maadili ya Utumishi wa Umma, wizi, uzembe na kushindwa kutekeleza majukumu na kusababisha hasara kwa Mwajiri. 

Kurasa za Karibu

Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.