Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais
Tume ya Utumishi wa Umma
Mhandisi Kelvin Chuma kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) leo ameongoza kikao cha "site meeting" kuhusu mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma unaoendelea katika mji wa Serikali Mtumba, Dodoma. Kikao kimefanyika eneo la mradi mji wa Serikali, Mtumba ambapo pamoja na mambo mengine mkandarasi CRJE (EA) LTD amewasilisha taarifa ya utekelezaji na hatua iliyofikiwa katika mradi huu.
Kaimu Katibu wa Tume, Bw. John Mbisso ameshiriki katika kikao hicho na ametembelea mradi kuona kazi inayoendelea kufanyika na hatua iliyofikiwa.
Hakimiliki © 2014. Tume ya Utumishi wa Umma. Haki zote zimehifadhiwa.